Na: Shalua Mpanda
Timu ya mpira wa wavu upande wa wanawake kutoka Halmashauri ya Jiji la Dar es salaam imeendeleza ubabe kwa timu zinazoshiriki mashindano ya Shirikisho la Michezo la Serikali za Mitaa Tanzania (SHIMISEMITA) mkoani Tanga mara baada ya kuigalagaza timu ya Halmashauri ya Manispaa ya Geita kwa seti 3-0.
Mchezo huo uliofanyika leo Agosti 27,2025 katika viwanja vya Shule ya Sekondari ya Ufundi Tanga(Tanga Tech),ulishuhudia timu ya Dar. City ikiongoza kwa seti zote tatu kwa 24-25,20-25,14-25.
Kwa ushindi huo umeifanya timu hiyo kufanikiwa kutinga hatua ya fainali ya michezo hiyo kwa upande wa Volleyball(wanawake) na kusubiri mshindi katika mechi ya leo baadae kati ya Dodoma na Hanang.
Dar City imezidi kujihakikishia medali na makombe zaidi mara baada ya kufanya vizuri katika michezo mingine ikiwemo riadha, mbio za kupokezana vijiti, kwaya, Darts na mengineyo.
1 BARABARA YA MOROGORO 11882 DAR ES SALAAM
Anuani ya Posta: S.L.P 20950
Simu ya mezani: 0738 378 386
Namba ya Mkononi: 0738 378 386
Barua Pepe: info@dcc.go.tz
Hatimiliki © 2017 Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam. Haki Zote Zimehifadhiwa.