Ninayo furaha kukuaribisha katika tovuti rasmi ya Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam ambapo tunaamini wananchi, wadau wa maendeleo, wawekezaji, watalii na wageni mbalimbali wanapata taarifa za kuaminika na kwa ukamilifu kuhusu dhamira ya Halmashauri ya Jiji ya kujenga Jiji lenye maendeleo endelevu yanayosimamiwa kwa kanuni za utawala bora ambao wananchi wanaishi katika kiwango bora cha maisha na kuwa na Jiji lenye mazingira mazuri yanayo himili ushindani na kuvutia wawekezaji.
Tunajivunia Jiji letu "Bandari Salama" na huduma mbalimbali tunazotoa kwa wananchi wetu. Tunashukuru kwa kutembelea tovuti yetu na tunaamini kuwa umenufaika kwa taarifa mbalimbali za utekelezaji serikalini, nakuhakishia kuwa tutaendelea kuboresha na kuhuisha tovuti hii kwa taarifa mbalimbali kadri muda unavyokwenda ili kukidhi matarajio yako kwa ubora wa hali ya juu.
1 BARABARA YA MOROGORO 11882 DAR ES SALAAM
Anuani ya Posta: S.L.P 9084
Simu ya mezani: +255 22 2123346
Namba ya Mkononi: 0715046974
Barua Pepe: cd@dcc.go.tz
Hatimiliki © 2017 Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam. Haki Zote Zimehifadhiwa.