Mradi wa Uimarishaji Mifumo ya Sekta za Umma (PS3) kwa kushirikiana na Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa pamoja na Wakala ya Serikali Mtandao (eGA) wamewezesha uzinduzi rasmi wa kitaifa wa tovuti mpya za Mikoa yote 26 ya Tanzania Bara, na Mamlaka za Serikali za Mitaa 185. Uzinduzi huo ulifanywa na Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa, Mh. George SImbachawene (Mb), na kuhudhuriwa na Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mh. Dkt. Harrison Mwakyembe (Mb), na Mkurugenzi Msaidizi wa USAID Tanzania, Tim Donnay, ambao ndio wafadhili wa Mradi wa PS3.
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Mhe. Paul C. Makonda akisikiliza kero za wafanyabiashara katika Shirika la Masoko Kariakoo
Wajumbe wa Kamati ya Huduma za Jamii wa Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam wakiongozwa na Mwenyekiti wa Kamati hiyo Bi. Leyla Hussein Madibi, Mstahiki Meya wa Jiji la Dar es Salaam, Isaya Mwita Charles pamoja na Waheshimiwa Madiwani na Wajumbe wa Kamati hiyo wamefanya ziara ya kuvitembelea vikundi vya kina mama na vijana vinavyonufaika na mikopo inayotolewa na Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam kwa vikundi hivyo.
Hatimiliki © 2017 Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam. Haki Zote Zimehifadhiwa.