Kituo Kikuu cha Mabasi Ubungo kilianzishwa na Tume ya Jiji la Dar es salaam na kufunguliwa rasmi na Mheshimiwa Benjamin William Mkapa, Rais Mstaafu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania tarehe 6 Disemba, 1999.
Kituo hicho kina ukubwa wa hekta 8.2 na uwezo wa kuhudumia jumla ya mabasi 637 kwa siku ambapo kati yake mabasi makubwa ni 291 na madogo 346. Kituo hicho pia hutoa huduma kwa wasafiri, wasindikizaji na watoa huduma mbalimbali wasiopungua 30,000 kwa siku.
Madhumuni ya kuanzishwa kwa kituo hicho yalikuwa ni kuondoa msongamano wa magari katikati ya Jiji la Dar es Salaam uliosababishwa na mabasi yaendayo mikoani na nchi jirani kuegesha pembezoni mwa barabara za Msimbazi, Bibi Titi Mohamed (Mnazi mmoja) na Morogoro (Eneo la Kisutu). Kituo hicho pia kilianzishwa ili kuwa chanzo cha mapato cha Halmashauri ya Jiji.
1 BARABARA YA MOROGORO 11882 DAR ES SALAAM
Anuani ya Posta: S.L.P 20950
Simu ya mezani: 2128800
Namba ya Mkononi:
Barua Pepe: info@dcc.go.tz
Hatimiliki © 2017 Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam. Haki Zote Zimehifadhiwa.