Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam katika mwaka huu wa fedha imetenga fedha za ujenzi wa Kituo Kikuu cha mabasi yaendayo mikoani na nchi jirani cha Mbezi Luis ili kupisha ujenzi wa miundombinu ya DART ndani ya Kituo Kikuu cha Mabasi cha Ubungo na kupunguza msongamano wa magari katika eneo la Ubungo.
Katika kutekeleza mradi huu, Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam, imekamilisha maandalizi ya uandaaji wa taarifa mbalimbali kuhusu mradi kama:
Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam pia imefanikiwa kupangiwa fedha za Serikali Kuu kwa ajili ya miradi ya kimkakati kiasi cha shilingi 50,689,000,000.00 ili kuweza kutekeleza ujenzi wa miundombinu wa Kituo Kikuu cha Mabasi yaendayo mikoani na nchi jirani cha Mbezi Luis.
Mradi utakapokamilika unatarajia kuiingizia Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam wastani wa Tsh.7 Bilioni kwa mwaka.
Michoro ya mwonekano wa Kituo kipya na cha kisasa cha mabasi yaendayo mikoani na nchi jirani cha Mbezi Luis baada ya ujenzi kukamilika
Picha zinazoonesha utekelezaji wa mradi wa ujenzi wa Kituo kipya na cha kisasa cha mabasi yaendayo mikoani na nchi jirani katika eneo la Mbezi Luis
1 BARABARA YA MOROGORO 11882 DAR ES SALAAM
Anuani ya Posta: S.L.P 20950
Simu ya mezani: 0738 378 386
Namba ya Mkononi: 0738 378 386
Barua Pepe: info@dcc.go.tz
Hatimiliki © 2017 Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam. Haki Zote Zimehifadhiwa.