Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam imejenga jengo la maegesho la ghorofa nane kwa njia ya ubia na Mfuko wa Jamii wa Parastatal Pension Fund (PPF) kwenye kiwanja chake kilichopo katika eneo la makutano ya Barabara ya Morogoro na Sokoine. Jengo hili lina uwezo wa kuegesha magari zaidi ya 376 na sehemu ya chini yenye ukubwa wa mita za mraba 185 kwa ajili ya ofisi. Kwa mujibu wa mkataba wake na PPF, Halmashauri ya Jiji inamiliki asilimia 50 na asilimia 50 zingine zinamilikiwa na PPF.
1 BARABARA YA MOROGORO 11882 DAR ES SALAAM
Anuani ya Posta: S.L.P 20950
Simu ya mezani: 2128800
Namba ya Mkononi:
Barua Pepe: info@dcc.go.tz
Hatimiliki © 2017 Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam. Haki Zote Zimehifadhiwa.