Na: Shalua Mpanda - Tanga
Waziri wa Viwanda na Biashara Mheshimiwa Dkt. Selemani Jafo amefungua mkutano mkuu wa nne wa Chama Cha Maafisa Biashara Wanawake Tanzania (TAWTO) unaofanyika hoteli ya Kiboko mkoani Tanga.
Akifungua mkutano huo leo Agosti 20,2025, Mhe. Jafo ameonesha kuchukizwa na baadhi ya Wakurugenzi wa Halmashauri nchini kutowapa kipaumbele maafisa biashara katika kutekeleza majukumu yao ya kazi.
Akijibu risala ya Mwenyekiti wa Chama hicho Bi. Elizabeth Swagi aliyetoa ombi kwa Waziri Jafo kuhusu vitendea kazi hasa kukosekana kwa magari kwa maafisa biashara hao, Waziri huyo wa Viwanda na Biashara amesema sio sawa kwa maafisa biashara kutokuwa na usafiri wa kwenda kufanyia kazi zao ukizingatia wao ndio wakusanyaji wakubwa wa mapato ya Halmashauri.
"Hili nalichukua kwa uzito mkubwa na tutashirikiana na TAMISEMI kuhakikisha maafisa biashara kote nchini wanapata magari ya kuwawezesha kufanya kazi zao, haiwezekani wakuu wengine wa Idara wanakuwa na magari na hawa wanaowezesha Halmashauri kupata mapato, hawana magari". Alisema
Awali akimkaribisha Waziri Jafo, Mkuu wa mkoa wa Tanga Dkt. Batilda Burian amemueleza Waziri huyo kuwa Mkutano huo wa maafisa biashara wanawake Tanzania utaleta chachu ya utendaji kazi kwa maafisa hao.
Mkutano huo mkuu wa nne wa Chama hicho una kauli mbiu isemayo "Mwanamke mpambanaji ni nguzo ya Maendeleo,Tushiriki vyema Uchaguzi Oktoba 2025".
1 BARABARA YA MOROGORO 11882 DAR ES SALAAM
Anuani ya Posta: S.L.P 20950
Simu ya mezani: 0738 378 386
Namba ya Mkononi: 0738 378 386
Barua Pepe: info@dcc.go.tz
Hatimiliki © 2017 Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam. Haki Zote Zimehifadhiwa.