Na: Shalua Mpanda
Kutokana na changamoto mbalimbali za kisheria zinazowakabili wananchi hasa wa mkoa wa Dar es salaam, Wizara ya Katiba na Sheria kupitia kampeni ya "Mama Samia Legal Aid" itaendesha zoezi la kutoa msaada wa kisheria kwa siku 10 mfululizo kuanzia Jumatatu Juni 16, 2025.
Hayo yameelezwa na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Mheshimiwa Albert Chalamila wakati akizungumza na waandishi wa Habari kuelekea uzinduzi wa Kampeni hiyo ndani ya mkoa huu unaotarajiwa kufanyika katika viwanja vya Maturubai Mbagala ambapo mgeni rasmi anatarajiwa kuwa Waziri Mkuu Mhe. Kassim Majaliwa (MB).
"Napenda niwafahamishe wakazi wa mkoa wa Dar es salaam kuwa kampeni hii itazinduliwa siku hiyo na baada ya hapo itaendelea katika Halmashauri zote ndani ya mkoa huu". Alisema Mhe.Chalamila.
Aidha, amesema katika zoezi hilo huduma zote zinazohusu msaada wa kisheria zikiwemo Mirathi,Migogoro ya adhi,Ndoa,uandishi wa wosia pamoja na nyingine zitatolewa na wataalamu wa masuala ya Sheria.
Naye Mkurugenzi wa Huduma za kisheria kutoka Wizara ya Katiba na Sheria Bi.Ester Msambazi amesema kutokana na changamoto zilizopo katika Jamii kuhusu uelewa wa masuala ya kisheria,Serikali iliamua kuanzisha kampeni hiyo ya "Mama Samia Legal Aid" ili kuwsaidia wale ambao hawana uwezo wa kupata huduma hizo.
Kampeni hii itakuwa no msaada mkubwa kwa Wananchi ambao wengi wao wanashindwa kupata huduma za kisheria kutokana na kipato au kutokuwa na uelewa juu ya masuala hayo.
1 BARABARA YA MOROGORO 11882 DAR ES SALAAM
Anuani ya Posta: S.L.P 20950
Simu ya mezani: 0738 378 386
Namba ya Mkononi: 0738 378 386
Barua Pepe: info@dcc.go.tz
Hatimiliki © 2017 Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam. Haki Zote Zimehifadhiwa.