Na Mariam Muhando.
Mkuu wa Wilaya ya Ilala Mhe. Edward Mpogolo amesema wamefanya tafakuri ya mafanikio alioyafanya Rais Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan hususani kwenye Sekta ya Elimu Sekondari ambapo wamepokea zaidi ya Bilioni 36 katika kuboresha miundombinu kwa kujenga shule na maeneo mengine.
Mhe. Mpogolo ameyasema hayo leo Juni 12, 2025 wakati wa kikao kazi cha maelekezo ya utekelezaji wa Miradi ya Sekta ya Elimu Sekondari kwa Wakuu wa Shule na Maafisa Elimu Kata Kwa lengo la kufanya tathmini ya utekelezaji wa Miradi hiyo katika kipindi cha mwaka wa fedha 205/2026 kilichofanyika kwenye Ukumbi wa Shule ya Sekondari ya Azania.
Mkuu huyo wa Wilaya amesema walikuwa wakikabiliwa na changamoto ya ukamilishwaji wa miradi kwa wakati ikiwemo lakini sasa miradi hiyo inaenda kwa kasi na ana imani kuwa itakamilika kwa wakati.
"Mheshimiwa Rais ametuletea fedha kwa ajili ya ujenzi wa shule mpya, ukarabati wa madarasa pia ametuletea zaidi ya Bilioni 1 kwa ajili ya ununuzi wa meza na viti na hivi vyote vimekamilika hivyo nampongeza Mkurugenzi wa Jiji hili kukamilisha miradi hiyo".Alisema Mhe. Mpogolo.
Naye Mkurugenzi wa Jiji la Dar es Salaam Ndugu Elihuruma Mabelya amesema Halmashauri ya Jiji iimetenga zaidi ya Shilingi Bilioni 6.2 ili ziweze kutekeleza ujenzi na uboreshaji wa miundombinu ya Jiji katika kipindi cha mwaka wa fedha 2025/2026.
"Namshkuru Mkuu wa Wilaya ya Ilala kwa kazi kubwa anayoifanya ikiwemo ya hamasa na usimamizi wa utekelezaji wa shughuli za Jiji hili na kupata mafanikio kwani tumeshuhudia matokea mazuri yanayoendelea kupatikana "Alisema Mabelya.
Kikao hicho kimejikita kutathmini, kuhakiki mapungufu yaliojitokeza katika utekelezaji wa miradi ili kuweza kujiandaa na mwaka wa fedha 2025/2026.
1 BARABARA YA MOROGORO 11882 DAR ES SALAAM
Anuani ya Posta: S.L.P 20950
Simu ya mezani: 0738 378 386
Namba ya Mkononi: 0738 378 386
Barua Pepe: info@dcc.go.tz
Hatimiliki © 2017 Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam. Haki Zote Zimehifadhiwa.