Na: Doina Mwambagi
Mkuu wa Wilaya ya Ilala, Mheshimiwa Edward Mpogolo, ameahidi kusimamia kwa ukaribu utekelezaji wa mpango wa utoaji wa mikopo ya asilimia 10 kutoka kwa mapato ya ndani, ikiwa ni utekelezaji wa malengo ya Serikali ya Awamu ya Sita ya Mheshimiwa Rais Samia Suluhu Hassan, ya kuwawezesha wanawake, vijana, na watu wenye ulemavu kiuchumi.
Akizungumza katika Kongamano la Jukwaa la Wanawake Wajasiriamali Ilala lililofanyika Leo tarehe 14 Juni 2025 katika Ukumbi wa Diamond Jubilee, DC Mpogolo amesema kuwa mkopo huu ni sehemu ya mikakati mikuu ya Serikali ya Awamu ya Sita ambayo inalenga kuwezesha wanawake kuwa na nguvu za kifedha na kujikwamua kiuchumi.
“Serikali ya Awamu ya Sita imetupa maelekezo thabiti kuhakikisha mikopo hii inawafikia walengwa hasa wanawake, vijana, na watu wenye ulemavu. Tutaendelea kusimamia kwa karibu utekelezaji wake kwa uwazi na usawa bila kupendelea wala kuangalia upande wowote,” amesema DC Mpogolo.
Kwa upande wake, Mkurugenzi wa Jiji la Dar es Salaam, Ndugu Elihuruma Mabelya, amesema kuwa zaidi ya shilingi bilioni 5 zinaenda kuwanufaisha wanawake, jambo linaloonyesha jitihada za serikali kuimarisha nafasi ya mwanamke katika uchumi wa taifa huku akisistiza kuwa maandalizi ya utoaji rasmi wa mikopo kwa vikundi vilivyoidhinishwa yamekamilika, na mchakato utaanza kwa kufuata sheria, kanuni mpya, na mfumo wa kibenki.
Mikopo ya asilimia 10 ni jitihada za Serikali ya Awamu ya Sita za kuleta maendeleo endelevu kwa wanawake, vijana, na watu wenye ulemavu.
1 BARABARA YA MOROGORO 11882 DAR ES SALAAM
Anuani ya Posta: S.L.P 20950
Simu ya mezani: 0738 378 386
Namba ya Mkononi: 0738 378 386
Barua Pepe: info@dcc.go.tz
Hatimiliki © 2017 Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam. Haki Zote Zimehifadhiwa.