Na Mariam Muhando
Mkuu wa Wilaya ya Ilala Mhe. Edward Mpogolo amewataka Viongozi wa Jiji la Dar es Salaam kuhakikisha mitaa yote 159 na kata 36 ndani ya jiji hilo, wanashiriki katika zoezi la usafi ,ili kuweka jiji hilo kuwa safi na salama.
Mhe. Mpogolo ametoa wito huo Mei 3, 2025 mara baada ya kukamilisha zoezi la usafi lililofanyika maeneo mbalimbali ya Jiji hili ikiwemo eneo la Fukwe za Dengu kwa kushirikiana na Wananchi na Makampuni ya usafi, zoezi ambalo linatekekezwa jumamosi kila wiki.
Mhe. Mpogolo amesema Jiji limekua likikabiliwa na changamoto ya takataka kwenye fukwe hasa eneo la Dengu na Feri, kutokana na kutupwa taka kwenye mito.
"Usafi ni jukumu la kila mmoja wetu, na kila Kiongozi alieomba dhamana ya kuongoza kwani sisi Viongozi tunao wajibu wa kuonyesha mfano katika maeneo yetu yanakuwa safi, Hivyo niwasihi wenzangu tuhakikishe Jiji hili linakuwa safi ambapo mvua zimeanza kupungua", Alisema Mhe. Mpogolo.
Wakati huo huo, amemtaka Mkurugenzi wa Jiji la Dar es Salaam kuweka Mpango wa kudumu wa kufanya Usafi katika fukwe zilizopo bahari ya Hindi ikiwemo eneo la Dengu kwani ndio eneo korifi linalopokea uchafu.
Nae Kaimu Mkurugenzi wa Jiji Wakili Faraja Nakuja amesema kwa kushirikiana na Wadau wa Usafi wanao mkakati wa kufanya Usafi kwa pamoja Kila wiki Kwa kuweka vitendedea kazi vitakavyosaidia kuboresha zoezi hilo.
"Hali yetu ya usafi itaendelea kuimarika kwani hili zoezi ni endelevu litakua likifanyika katika maeneo mbalimbali ya Jiji ili kuweza kuimarika na kuwavutia wenyeji na wageni pindi wanapoingia hapa Nchini". Alisema Wakili Nakua.
1 BARABARA YA MOROGORO 11882 DAR ES SALAAM
Anuani ya Posta: S.L.P 20950
Simu ya mezani: 0738 378 386
Namba ya Mkononi: 0738 378 386
Barua Pepe: info@dcc.go.tz
Hatimiliki © 2017 Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam. Haki Zote Zimehifadhiwa.