Katibu Tawala wa Mkoa wa Dar es Salaam ndugu Abdul Mhinte leo hii amekutana na watumishi wa Halmashauri ya Jiji la Dar es salaam Makao Makuu kwa lengo la kujitambulisha mara baada ya miezi kadhaa ya kuteuliwa kushika nafasi hiyo katika mkoa wa huu.
Akizungumza na Watumishi hao wwkiongozwa na Katibu Tawala Wilaya ya Ilala Bi. Charangwa Selemani na Mkurugenzi wa Jiji Elihuruma Mabelya, Katibu Tawala huyo wa Mkoa amesema lengo kuu la Halmashari ni kukusanya mapato na utekelezaji wa miradi ya maendeleo.
Amesema imefika wakati sasa Halmashauri kujikita zaidi kwenye ukusanyaji wa mapato kwa kutumia teknolojia ili kuweza kuwafikia walipaji wengi zaidi na kupunguza kazi za ufuatiliaji.
Baadhi ya watumishi waliopata nafasi ya kuongea katika kikao hicho, wamempongeza Mkurugenzi wa Jiji hili kwa kuwa msikivu katika baadhi ya mambo wanayopeleka kwake katika shughuli zao za kila siku.
"Dunia ya sasa hivi ni ya Sayansi na Teknolojia, vivyo hivyo hata kwenye suala la ukusanyaji wa mapato ni lazima tutumie teknolojia kwa kuwa Dunia ndipo inapoenda huko’. Alisisitiza
Akizungumza wakati wa kumkaribisha mgeni Rasmi,Katibu Tawala wilaya ya Ilala Bi. Charangwa alisema kuwa Halmashauri ya Jiji la Dar es salaam kwa sasa inakwenda kasi katika miradi ya maendeleo huku akimshukuru Mhe. Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kuendelea kuleta fedha nyingi za Miradi katika Wilaya hii.
Kikao hiki ni cha kwanza kwa Katibu Tawala huyo kwa Watumishi hao toka ateuliwe na Mhe. Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan takribani miezi miwili iliyopita.
1 BARABARA YA MOROGORO 11882 DAR ES SALAAM
Anuani ya Posta: S.L.P 20950
Simu ya mezani: 0738 378 386
Namba ya Mkononi: 0738 378 386
Barua Pepe: info@dcc.go.tz
Hatimiliki © 2017 Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam. Haki Zote Zimehifadhiwa.