Na: Shalua Mpanda
Msafara wa viongozi kutoka Jiji la Chengdu mkoa wa Schuan nchini China umetembelea Halmashauri ya jiji la Dar es salaam ili kuanzisha mahusiano mbalimbali yakiwemo ya kibiashara, elimu, kilimo nk.
Msafara huo ulioongozwa na Naibu Mkurugenzi wa Kamati ya Kudumu ya Bunge la Chengdu na Naibu Meya, Bw. Wang Pingjiang ambapo ulipokelewa na Mkuu wa wilaya ya Ilala Edward Mpogolo na Mkurugenzi wa Jiji Elihuruma Mabelya.
Katika mazungumzo yao yaliyotumia takribani saa mbili, ujumbe wa viongozi hao kutoka Jiji hilo la nne kwa ukubwa nchini China walionesha kuvutiwa na namna Jiji la Dar es salaam linavyoendelea kwa kasi katika miundombinu.
'Hii ni mara yetu ya kwanza kufika Tanzania na imekuwa bahati katika nchi zote za Afrika, tunatembelea katika majiji mawili tu mojawapo ni hili la Dar e salaam'. Alisema Bw. Pingjiang
Kwa upande wake Mkuu wa wilaya ya Ilala Edward Mpogolo amesema ushiriano baina ya nchi hizi mbili uliasisiwa na viongozi wakuu Hayati Baba wa Taifa Mwl. Julius Kambarage Nyerere na kiongozi wa Taifa la China Mao Tse - Tung hivyo hawana budi kuuendeleza.
Mkurugenzi wa Jiji hili Elihuruma Mabelya ameainisha maeneo ambayo angependa washirikiane nao katika kubadilishana ujuzi kuwa ni Elimu, Uwekezaji, Utunzaji wa Mazingira na miundombinu.
Jiji la Chengdu ni moja ya majiji makubwa nchini China ambapo mpaka kufikia mwaka 2023 ilikadiriwa kuwa na wakazi milioni 21 ambapo ni kitovu cha uchumi, teknolojia, fedha, na miundombinu ya usafiri likiwa na viwanja viwili vya ndege vya kimataifa,
1 BARABARA YA MOROGORO 11882 DAR ES SALAAM
Anuani ya Posta: S.L.P 20950
Simu ya mezani: 0738 378 386
Namba ya Mkononi: 0738 378 386
Barua Pepe: info@dcc.go.tz
Hatimiliki © 2017 Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam. Haki Zote Zimehifadhiwa.