Na: Shalua Mpanda - Tanga
Halmashauri ya Jiji la Dar es salaam imeendeleza ubabe kwa timu zinazoshiriki mashindano ya SHIMISEMITA yanayoendelea mkoani Tanga baada ya timu ya mpira wa mikono(Handball) upande wa wanawake kuishushia kichapo timu ya Halmashauri ya wilaya ya Kishapu kwa magoli 8-2 katika mchezo uliochezwa kwenye uwanja wa shule ya Sekondari Usagara.
Kipindi cha kwanza kilionekana kigumu kwa timu zote mbili kushambuliana kwa tahadhari na kufanya timu hizo kwenda mapumziko zikiwa zimefungana goli 1-1.
Kipindi cha pili kilianza kwa kasi na alikuwa mchezaji wa timu ya Jiji la Dsm Martha Maurice aliyeonekana mwiba mchungu kwa timu ya Kishapu baada ya kuchangia magoli manne kati ya manane yaliyofungwa.
Magoli mengine yalifungwa na Bertha ambaye alifunga mawili, Cassiana goli moja na nahodha wa timu Rehema aliyechangia goli moja katika ushindi huo mnono.
Michezo mingine inayosubiriwa kupigwa leo hii Agosti 17,2025 ni mchezo wa mpira wa miguu kati ya Jiji la Dsm na Kibondo na mpira wa mikono(wanaume) kati ya Jiji la Dsm na Tanga Jiji.
Mashindano hayo yanayoshirikisha halmashauri zote nchini yenye kauli mbiu "Jitokeze Kupiga Kura kwa Maendeleo ya Michezo" yameanza rasmi Agosti 15 na yanatarajiwa kukamilika Agosti 29 mwaka huu.
1 BARABARA YA MOROGORO 11882 DAR ES SALAAM
Anuani ya Posta: S.L.P 20950
Simu ya mezani: 0738 378 386
Namba ya Mkononi: 0738 378 386
Barua Pepe: info@dcc.go.tz
Hatimiliki © 2017 Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam. Haki Zote Zimehifadhiwa.