Na: Aritha Mziray-Tanga
Timu ya mpira wa miguu ya Halmashauri ya Jiji la Dar es salaam imegawana pointi na timu kutoka Halmashauri ya wilaya ya musoma mara baada ya kutoka sare ya goli 1-1 katika mchezo mkali wa mashindano ya SHIMISEMITA mkoani Tanga.
Goli hilo lililofungwa na mchezaji hatari lazaro kajole ndani ya dakika ya tatu za kipindi cha kwanza cha mchezo huo uliochezwa katika uwanja wa shule ya Sekondari Galanos.
Kipindi cha pili timu zote zilifanya mabadiliko ya wachezaji ambao kwa upande wa musoma iliweza kuwaongezea nguvu na kupata goli la penati katika dakika ya 33 ya mchezo huo.
Timu hiyo imejikusanyia pointi 5 katika kundi lao mara baada ya kushinda mchezo wa kwanza dhidi ya timu ya Handeni Tc.
Mashindano hayo yanayoshirikisha halmashauri zote nchini yenye kauli mbiu "Jitokeze Kupiga Kura kwa Maendeleo ya Michezo" yameanza rasmi Agosti 15 na yanatarajiwa kukamilika Agosti 29 mwaka huu.
1 BARABARA YA MOROGORO 11882 DAR ES SALAAM
Anuani ya Posta: S.L.P 20950
Simu ya mezani: 0738 378 386
Namba ya Mkononi: 0738 378 386
Barua Pepe: info@dcc.go.tz
Hatimiliki © 2017 Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam. Haki Zote Zimehifadhiwa.