Na: Shalua Mpanda-Tanga
Timu ya mpira wa miguu ya Halmashauri ya Jiji la Dar es salaam imegawana pointi na timu kutoka Halmashauri ya wilaya ya Kibondo ya mkoani Kigoma mara baada ya kutoka sare ya goli 1-1 katika mchezo mkali wa mashindano ya SHIMISEMITA mkoani Tanga.
Ilikuwa ni timu ya Halamshauri ya Jiji la Dar es salaam iliyoanza kuona lango la mpinzani wake dakika ya 29 kwa njia ya mkwaju wa penati mara baada ya mchezaji wa timu hiyo kufanyiwa madhambi na beki wa timu ya Kibondo.
Goli hilo lililofungwa na mchezaji hatari Ernest Tyson lilidumu hadi dakika 45 za kipindi cha kwanza cha mchezo huo uliochezwa katika uwanja wa shule ya Sekondari Galanos.
Kipindi cha pili timu zote zilifanya mabadiliko ya wachezaji ambao kwa upande wa Kibondo iliweza kuwaongezea nguvu na kupata goli la kusawazisha katika dakika ya 89 ya mchezo huo.
Katika mchezo huo mchezaji wa timu ya Halmashauri ya Jiji la Dsm Idrisa Miraji alioneshwa kadi ya pili ya njano iliyompelekea kupata kadi nyekundu na kutolewa nje kwa kile mwamuzi wa mchezo huo alichodai kuwa anachelewesha muda.
Timu hiyo imejikusanyia pointi 4 katika kundi lao mara baada ya kushinda mchezo wa kwanza dhidi ya timu ya Handeni Tc.
1 BARABARA YA MOROGORO 11882 DAR ES SALAAM
Anuani ya Posta: S.L.P 20950
Simu ya mezani: 0738 378 386
Namba ya Mkononi: 0738 378 386
Barua Pepe: info@dcc.go.tz
Hatimiliki © 2017 Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam. Haki Zote Zimehifadhiwa.