Na.Judith Msuya na Amanzi Kimonjo
Wajumbe wa Kamati ya Fedha na Utawala ya Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam leo Februari 17, 2022 wamefanya ziara ya kutembelea miradi ya maendeleo iliyotekelezwa na Halmashauri hiyo kwa kipindi cha robo ya pili (Oktoba - Desemba, 2021) lengo likiwa ni kufanya tathimini ya miradi hiyo jinsi inavyotekelezwa.
Wakiwa kwenye ziara hiyo iliyoongozwa na mwenyekiti wa kamati ambaye ni Mstahiki Meya wa Halmashauri ya Jiji la Dae es Salaam Mhe.Omary Kumbilamoto kamati iliweza kutembelea miradi ya ujenzi wa vituo vya afya ikiwemo ujenzi wa Kituo cha afya Kinyerezi pamoja na ujenzi wa Kituo cha Afya Kipunguni ambapo Kituo cha afya Kinyerezi chenye majengo mawili ikiwemo jengo la Mama na mtoto pamoja na jengo la upasuaji kinajengwa kwa kutumia Fedha za mapato ya ndani takribani shilingi milioni 300 kikiwa hatua ya msingi na kinatarajiwa hadi kufikia tarehe 30,Aprili 2022 kituo hicho kinatarajiwa kukamilika huku Kituo cha Afya kipunguni kinachojengwa kwa kutumia Fedha za tozo takribani shilingi milioni 250 kikiwa hatua ya kumwaga jamvi na hadi kufikia Aprili 2022 kituo hicho kinatarajiwa kukamilika.
Akizungumza katika majumuisho ya ziara hiyo kwa niaba ya Mstahiki Meya wa Halmadhauri ya Jiji la Dar es Salaam Naibu Meya wa Jiji la Dar es Salaam Mhe. Saady Khimji "amesema nifaraja kwetu kuona kile tunachoazimia katika vikao vyetu kinatekelezwa niwaombe tuu wataalamu wetu wakitekeleza miradi hii wakumbuke kuwashirikisha wananchi wa eneo husika ambapo mradi unatekelezwa.
"Sambamba na hilo Mhe. Khimji ameendelea kusema Napenda kumpongeza Mkurugenzi wa Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam pamoja na watumishi wote wa Halmashauri ya Jiji kwa namna ambavyo wanatupa ushirikiano na kuhakikisha tunapata maemdeleo katika kata zetu na hivyo kuimarisha huduma za wananchi wetu wa Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam.
Aidha Kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam ambaye ni Mganga Mkuu wa Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam Bi. Elizabeth Nyema ameweza kuwahakikishia wajumbe wa kamati ya Fedha na Utawala kutekeleza yote aliyoagizwa na kamati hiyo.
"Niwahakikishie tu kwamba tutaandaa kikao na timu nzima ya ujenzi ya Halmashauri ya Jiji pamoja na Kamati ya maendeleo ya Kata ili kuweka mambo vizuri baina yetu sisi ili miradi hii iweze kukamilika kwa wakati na kwa usanifu zaidi." Ameeleza Bi. Elizabeth.
1 BARABARA YA MOROGORO 11882 DAR ES SALAAM
Anuani ya Posta: S.L.P 20950
Simu ya mezani: 2128800
Namba ya Mkononi: 0713614364
Barua Pepe: info@dcc.go.tz
Hatimiliki © 2017 Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam. Haki Zote Zimehifadhiwa.