Na: Shalua Mpanda
Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Kassim Majaliwa amekemea vitendo vya ukatili wa aina mbalimbali unaoendela katika baadhi ya maeneo nchini huku akisisitiza Jamii kutokufumbia macho vitendo hivyo.
Akizungumza katika uzinduzi wa kampeni maalum ya msaada wa kisheria ya Mama Samia "Mama Samia Legal Aid" uliofanyika katika viwanja vya Maturubai wilayani Temeke, Waziri Mkuu Majaliwa amesema lengo la kuanzisha Kampeni hiyo ni kusogeza huduma za kisheria karibu na wananchi ili kuweza kumaliza changamoto hiyo.
Aidha, amesema Serikali imelenga kuhakikisha wananchi wote wanaendelea kupata haki bila upendeleo wowote na kuweza kuishi kwa amani na utulivu.
"Kuna aina mbalimbali za unyanyasaji katika Jamii,ondoeni uoga msiogope kwenda kutoa taarifa dhidi ya unyanyasaji unaotokea katika maeneo yenu". Alisisitiza Mhe. Majaliwa.
Kwa upande wake Waziri wa Katiba na Sheria Dkt. Damas Ndumbaro alisema kampeni hiyo imeweza kufikia mikoa 31 Tanzania Bara na Visiwani huku akieleza namna walivyojipanga kuanza awamu ya pili ya Kampeni hiyo.
Kampeni hii yenye kauli mbiu "Msaada wa Kisheria kwa Haki, Usawa, Amani na Maendeleo" ina lengo la kuwafikishia wananchi huduma za kisheria karibu ili kuweza kusaidia wananchi wasio na uwezo wa kupata huduma hizo kutokana na gharama.
1 BARABARA YA MOROGORO 11882 DAR ES SALAAM
Anuani ya Posta: S.L.P 20950
Simu ya mezani: 0738 378 386
Namba ya Mkononi: 0738 378 386
Barua Pepe: info@dcc.go.tz
Hatimiliki © 2017 Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam. Haki Zote Zimehifadhiwa.