• Wasiliana Nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua Pepe za Watumishi |
    • Malalamiko |
Dar es Salaam City Council
Dar es Salaam City Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Mamlaka za Serikali za Mitaa Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia ya Jiji
    • Dira na Dhamira
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati ya Halmashauri
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Idara
      • Fedha, Utawala na Utumishi
      • Ujenzi na Zimamoto
      • Udhibiti Taka
      • Mipangomiji, Mazingira na Usafirishaji
      • Afya na Huduma za Tiba
    • Vitengo
      • Mipango, Ufuatiliaji na Takwimu
      • Sheria na Usalama
      • Itifaki, Uhusiano na Umma
      • Mkaguzi wa Ndani
      • Ugavi na Manunuzi
  • Fursa za Uwekezaji
    • Shughuli za Utalii
      • Dar es Salaam Yetu
      • Misitu na Mashamba ya wanyama wafugwao
      • Sehemu za kitamaduni, ngoma za asili na sanaa za mikono
      • Kituo cha Urithi wa Ubunifu Majengo na Utalii
      • Maeneo ya kupumzika, bustani na viwanja vya michezo
      • Maeneo ya Manunuzi
      • Majengo na maeneo ya kihistoria
      • Uwanda wa bahari, fukwe na visiwa
    • Urejelezaji wa Taka Ngumu
  • Huduma Zetu
    • Vibali vya Pikipiki
    • Vibali vya Maegesho ya Teksi
    • Vibali vya Kuingiza Magari ya Mizigo
    • Vituo Vikuu vya Mabasi
    • Udhibiti Taka Ngumu
    • Taarifa za Historia ya Viwanja
    • Mazishi ya miili ya marehemu wasiokuwa na ndugu
  • Madiwani
    • Orodha ya Madiwani
    • Kamati za Kudumu
      • Kamati ya Fedha na Uongozi
      • Kamati ya Mipangomiji, Mazingira na Miundombinu
      • Kamati ya Mipango na Ufuatiliaji
      • Kamati ya Huduma za Jamii
      • Kamati ya Maadili
    • Ratiba ya Vikao vya Kisheria
    • Ratiba ya Mstahiki Meya
    • Mameya Wazamani wa Jiji
  • Miradi
    • Miradi iliyokamilika
    • Miradi iliyo kwenye Mpango
    • Miradi Inayoendelea
    • Vitega Uchumi vya Jiji
  • Machapisho
    • Sheria
    • Sheria Ndogo
    • Sera
    • Miongozo
    • Taarifa mbalimbali
    • Fomu za Maombi
    • Fomu za Ahadi ya Uadilifu
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Vyombo vya Habari
    • Maktaba ya Picha
    • Maktaba ya Video
    • Hotuba
    • Habari Mpya
    • Matukio

"Tumechukua hatua za haraka kuhakikisha Barabara zinapitika tena" - Mkurugezni Mabelya

Tarehe iliyowekwa: April 2nd, 2025

Na: Shalua Mpanda

Mkurugenzi wa Jiji la Dar es salaam Elihuruma Mabelya amesema Wakala wa Barabara za Mijini na Vijijini (TARURA) kwa kushirikiana na Halmashauri ya Jiji wamedhamiria kuzifanyia ukarabati barabara na makaravati yaliyoathiriwa na mvua zinazoendelea kunyeesha katika maeneo mbalimbali.

Ameyasema hayo wakati wa ziara ya kukagua maeneo yalioathiriwa na mvua hizo katika kata za Mzinga na Kivule huku akisema Serikali ya awamu ya sita chini ya Mheshimiwa Rais Dkt Samia Suluhu imekuwa ikitoa fedha nyingi kila mwaka katika miundombinu ya barabara ndani ya Halmashauri hii.

"Leo hii tumefanya ziara katika eneo hili la daraja la Mzinga ambalo kwa siku kadhaa lilikuwa halipitiki kutokana na kukatika baada ya maji kukata eneo la barabara hii,niwahakikishie Halmashauri ya Jiji inachukua hatua za haraka kuhakikisha inarekebisha barabara zote zilizopata changamoto kama hii iii wananchi waendelee na shughuli zao za kuzalisha uchumi'. Alisisitiza.

Akiwa katika eneo la barabara ya Pugu Majohe Mbondole, Mkurugenzi huyo amesema Halmashauri ya Jiji kupitia fedha za  mapato yake ya ndani imeshaanza ujenzi wa barabara ya zege yenye urefu wa mita 400 na mchakato unaendelea kuhakikisha barabara hiyo yenye urefu wa takribani kilometa 12 inajengwa kwa kiwango cha lami kupitia Wakala wa Barabara za Mijini na Vijijini (TARURA).

Kwa upande wake Meneja wa TARURA wilaya ya Ilala Mhandisi  John Magori amesema  kiasi cha kilomita  400 za barabara za kiwango cha lami zimejengwa na Halmashauri kupitia fedha  za mapato yake ya ndani.

Aidha Mhandisi huyo amewaomba wananchi kuwa wavumilivu katika kipindi hiki cha mvua ambapo barabara nyingi zinakuwa na changamoto kutokana na maeneo maji kuharibu miundombinu hiyo huku akisisitiza kufanya kazi usiku na mchana kukabiliana na changamoto hiyo.

Ziara hiyo pia ilimhusisha Mkuu wa wilaya ya Ilala Mheshimiwa Edward Mpogolo ambaye amekuwa mstari wa mbele kila mara kufika  kwa wakati kila inapotokea dharura hasa katika miundombinu ya barabara.

Matangazo

  • TAARIFA KWA UMMA February 19, 2025
  • TAARIFA KWA UMMA - MATUMIZI YA NISHATI SAFI YA KUPIKIA January 17, 2025
  • MATOKEO YA UPIMAJI WA KITAIFA WA DARASA LA NNE (SFNA) 2024 January 04, 2025
  • UCHAGUZI WA WANAFUNZI WA KIDATO CHA KWANZA, 2025 December 16, 2024
  • Angalia zote

Habari Mpya

  • "Tutahakikisha tunasimamia Kata 36 na Mitaa 159 ili Jiji la DSM liwe safi" - DC Mpogolo

    May 03, 2025
  • Jiji La DSM laweka mikakati kushinda UMITASHUMTA ngazi ya Mkoa

    April 29, 2025
  • Wakazi wa Jiji la Dar es Salaam waadhimisha Muungano kwa kupanda miti na kufanya usafi wa mazingira

    April 26, 2025
  • Zoezi la usafi wa mwisho wa wiki laendelea

    April 12, 2025
  • Angalia zote

Video

Msimbazi Basin Development Project Implementation Area
Video Zingine

Viunganishi vya Haraka

  • Mameya wa zamani wa Jiji
  • Vibali vya kuingia na Pikipiki katikati ya Jiji
  • Udhibiti wa Taka ngumu Jijini
  • Eneo Maalum la Usafi Jijini
  • Kituo cha Urithi wa Ubunifu Majengo na Utalii
  • Uwanda wa Bahari, Fukwe na Visiwa
  • Sehemu za Kitamaduni, Ngoma za Asili na Sanaa za Mikono
  • Majengo na Maeneo ya Kihistoria
  • Maeneo ya Kupumzika, Bustani na Viwanja vya Michezo

Viunganishi Linganifu

  • BUNGE
  • Blogu ya Jiji
  • UTUMISHI
  • IKULU
  • TAMISEMI
  • IDARA YA HABARI MAELEZO

Wasomaji mbalimbali duniani

world map hits counter

Idadi ya Wasomaji

free HitCounter

Ramani ya Eneo

Wasiliana Nasi

    1 BARABARA YA MOROGORO 11882 DAR ES SALAAM

    Anuani ya Posta: S.L.P 20950

    Simu ya mezani: 0738 378 386

    Namba ya Mkononi: 0738 378 386

    Barua Pepe: info@dcc.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya Tovuti

Hatimiliki © 2017 Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam. Haki Zote Zimehifadhiwa.