• Wasiliana Nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua Pepe za Watumishi |
    • Malalamiko |
Dar es Salaam City Council
Dar es Salaam City Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Mamlaka za Serikali za Mitaa Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia ya Jiji
    • Dira na Dhamira
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati ya Halmashauri
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Idara
      • Fedha, Utawala na Utumishi
      • Ujenzi na Zimamoto
      • Udhibiti Taka
      • Mipangomiji, Mazingira na Usafirishaji
      • Afya na Huduma za Tiba
    • Vitengo
      • Mipango, Ufuatiliaji na Takwimu
      • Sheria na Usalama
      • Itifaki, Uhusiano na Umma
      • Mkaguzi wa Ndani
      • Ugavi na Manunuzi
  • Fursa za Uwekezaji
    • Shughuli za Utalii
      • Dar es Salaam Yetu
      • Misitu na Mashamba ya wanyama wafugwao
      • Sehemu za kitamaduni, ngoma za asili na sanaa za mikono
      • Kituo cha Urithi wa Ubunifu Majengo na Utalii
      • Maeneo ya kupumzika, bustani na viwanja vya michezo
      • Maeneo ya Manunuzi
      • Majengo na maeneo ya kihistoria
      • Uwanda wa bahari, fukwe na visiwa
    • Urejelezaji wa Taka Ngumu
  • Huduma Zetu
    • Vibali vya Pikipiki
    • Vibali vya Maegesho ya Teksi
    • Vibali vya Kuingiza Magari ya Mizigo
    • Vituo Vikuu vya Mabasi
    • Udhibiti Taka Ngumu
    • Taarifa za Historia ya Viwanja
    • Mazishi ya miili ya marehemu wasiokuwa na ndugu
  • Madiwani
    • Orodha ya Madiwani
    • Kamati za Kudumu
      • Kamati ya Fedha na Uongozi
      • Kamati ya Mipangomiji, Mazingira na Miundombinu
      • Kamati ya Mipango na Ufuatiliaji
      • Kamati ya Huduma za Jamii
      • Kamati ya Maadili
    • Ratiba ya Vikao vya Kisheria
    • Ratiba ya Mstahiki Meya
    • Mameya Wazamani wa Jiji
  • Miradi
    • Miradi iliyokamilika
    • Miradi iliyo kwenye Mpango
    • Miradi Inayoendelea
    • Vitega Uchumi vya Jiji
  • Machapisho
    • Sheria
    • Sheria Ndogo
    • Sera
    • Miongozo
    • Taarifa mbalimbali
    • Fomu za Maombi
    • Fomu za Ahadi ya Uadilifu
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Vyombo vya Habari
    • Maktaba ya Picha
    • Maktaba ya Video
    • Hotuba
    • Habari Mpya
    • Matukio

RC DSM Azindua Mkakati endelevu wa Usafi na Uhifadhi wa Mazingira

Tarehe iliyowekwa: November 22nd, 2021

Na. Judith Damas

Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mhe. Amos Makalla amezindua mkakati endelevu wa Usafi na uhifadhi wa mazingira Dar es salaam ambapo ameelekeza kila Mtendaji kusimamia Usafi na kuhakikisha sheria inatumika kutoa adhabu kwa wachafuzi wa mazingira, hayo ameyabainisha leo Novemba, 23 katika mkutano wa Uzinduzi wa Usafi na uhifadhi wa Mazingira Dar es Salaam  wenye kauli mbiu isemayo 'Safisha Pendezesha Dar es Salaam' uliofanyika katika  Ukumbi wa Mikutano wa Mwalimu Julius Nyerere Jijini Dar es Salaam, ukiwa umehudhuriwa na Viongozi mbalimbali wa kiserikali, Chama Cha Mapinduzi, Viongozi wa Dini, Wastahiki Meya, Vyombo vya ulinzi na usalama, Maafisa Mazingira, Wenyeviti na Watendaji wa Mitaa na wadau mbalimbali.

Akizungumza wakati wa uzinduzi huo, Mhe.  Makalla ametoa maelekezo 10 kwa Viongozi wote na wananchi wazingatie  ili kufanikisha Kampeni hiyo ikiwemo Kila Jumamosi ya mwisho wa mwezi kuwa siku ya Usafi wa pamoja "Kila Manispaa iteue wakandarasi wa Usafi Wenye Sifa na Vigezo, ikiwemo Vifaa vya kutosha vya kufanyia Usafi, Kila Manispaa kupitia upya Sheria za udhibiti wa Biashara holela na Usafi na Kama hazipo zitungwe, Kila Mwenyekiti na Mtendaji wa Mtaa kuhamasisha na kusimamia Usafi kwenye eneo lake, Mkataba na kila Manispaa kusimamia Usafi na Machinga wasirudi kwenye maeneo yaliyokatazwa, kila Taasisi kulinda maeneo yake  ili yasivamiwe na Machinga, Wakuu wa Wilaya kusimamia Usafi katika maeneo ya fukwe zote za Mkoa huo kufanyiwa Usafi na uwe endelevu, Amepiga marufuku tabia ya Wizi wa vyuma na minyororo iliyowekwa kwaajili ya kupendezesha mandhari ya Jiji(vigingi) pia ameeleza kuwa usafi unaendana na muonekano mzuri wa majengo hivyo ameelekeza majengo yote yapakwe rangi yawe na muonekano mzuri.

Sambamba na hayo Mhe. Makalla ametoa wito kwa Wananchi kuitumia siku ya tarehe 4 Desemba ambayo ndiyo siku ya  uzinduzi wa Usafi Kata ya Kivukoni kwa kufanya Usafi wa kina kwenye maeneo yao ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya Sherehe za Uhuru.

Kwa upande Mwingine Mhe. Makalla ameweza kuingia mkataba na Wakuu wa Wilaya pamoja na Wakurugenzi wote wa Kila Halmashauri kusimamia usafi na Kuhakikisha Wafanya biashara ndogondogo hawarudi tena katika maeneo yasiyo rasmi na maeneo hayo yafanyiwe usafi wa kina.

"Mkataba huu ulioambatana na mahudhurio kama makubaliano ya kutekeleza suala zima la usafi na uhifadhi wa mazingira utasainiwa na Mkuu wa Wilaya pamoja na Mkurugenzi wa kila Halmashauri na mkitoka hapa mhakikishe mnapitia sheria ndogondogo za usafi na kama hazipo mkazitunge, muende mkajifunze kwa wenzenu waliwezaje kufanikisha suala zima la usafi Katika Mikoa yao." Ameeleza Mhe. Makalla.

Naye Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi Mkoa wa DSM Bi. Cathe Kamba amempongeza Mkuu wa Mkoa wa DSM pamoja na Viongozi wake kwa kazi nzuri walioifanya ya kuwapanga wafanyabiashara ndogondogo maarufu kama Machinga kutoka sehemu zisizo rasmi na kwenda kufanya biashara maeneo rasmi hivyo ameahidi kushirikiana na viongozi hao katika kampeni ya usafi na uhifadhi wa mazingira Mkoa wa Dar es Salaam na kuhakikisha Mkoa unakua safi.

Akitoa shukrani zake Kwa Mkuu wa Mkoa Mwenyekiti wa Machinga  Bw. Masoud Issa amesema" Tunamshukuru Mkoa wa Mkoa Mhe. Makalla kwa kutushirikisha katika zoezi zima la kutupanga katika maeneo rasmi na kwaniaba ya Wamachinga wenzangu naahidi hatutomuangusha tutabaki katika maeneo rasmi na tutahakikisha tunafanya usafi na  tunahifadhi mazingira ili kuipendezesha Dar es Salaam."

Matangazo

  • TAARIFA KWA UMMA February 19, 2025
  • TAARIFA KWA UMMA - MATUMIZI YA NISHATI SAFI YA KUPIKIA January 17, 2025
  • MATOKEO YA UPIMAJI WA KITAIFA WA DARASA LA NNE (SFNA) 2024 January 04, 2025
  • UCHAGUZI WA WANAFUNZI WA KIDATO CHA KWANZA, 2025 December 16, 2024
  • Angalia zote

Habari Mpya

  • "Tutahakikisha tunasimamia Kata 36 na Mitaa 159 ili Jiji la DSM liwe safi" - DC Mpogolo

    May 03, 2025
  • Jiji La DSM laweka mikakati kushinda UMITASHUMTA ngazi ya Mkoa

    April 29, 2025
  • Wakazi wa Jiji la Dar es Salaam waadhimisha Muungano kwa kupanda miti na kufanya usafi wa mazingira

    April 26, 2025
  • Zoezi la usafi wa mwisho wa wiki laendelea

    April 12, 2025
  • Angalia zote

Video

Msimbazi Basin Development Project Implementation Area
Video Zingine

Viunganishi vya Haraka

  • Mameya wa zamani wa Jiji
  • Vibali vya kuingia na Pikipiki katikati ya Jiji
  • Udhibiti wa Taka ngumu Jijini
  • Eneo Maalum la Usafi Jijini
  • Kituo cha Urithi wa Ubunifu Majengo na Utalii
  • Uwanda wa Bahari, Fukwe na Visiwa
  • Sehemu za Kitamaduni, Ngoma za Asili na Sanaa za Mikono
  • Majengo na Maeneo ya Kihistoria
  • Maeneo ya Kupumzika, Bustani na Viwanja vya Michezo

Viunganishi Linganifu

  • BUNGE
  • Blogu ya Jiji
  • UTUMISHI
  • IKULU
  • TAMISEMI
  • IDARA YA HABARI MAELEZO

Wasomaji mbalimbali duniani

world map hits counter

Idadi ya Wasomaji

free HitCounter

Ramani ya Eneo

Wasiliana Nasi

    1 BARABARA YA MOROGORO 11882 DAR ES SALAAM

    Anuani ya Posta: S.L.P 20950

    Simu ya mezani: 0738 378 386

    Namba ya Mkononi: 0738 378 386

    Barua Pepe: info@dcc.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya Tovuti

Hatimiliki © 2017 Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam. Haki Zote Zimehifadhiwa.