• Wasiliana Nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua Pepe za Watumishi |
    • Malalamiko |
Dar es Salaam City Council
Dar es Salaam City Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Mamlaka za Serikali za Mitaa Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia ya Jiji
    • Dira na Dhamira
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati ya Halmashauri
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Idara
      • Fedha, Utawala na Utumishi
      • Ujenzi na Zimamoto
      • Udhibiti Taka
      • Mipangomiji, Mazingira na Usafirishaji
      • Afya na Huduma za Tiba
    • Vitengo
      • Mipango, Ufuatiliaji na Takwimu
      • Sheria na Usalama
      • Itifaki, Uhusiano na Umma
      • Mkaguzi wa Ndani
      • Ugavi na Manunuzi
  • Fursa za Uwekezaji
    • Shughuli za Utalii
      • Dar es Salaam Yetu
      • Misitu na Mashamba ya wanyama wafugwao
      • Sehemu za kitamaduni, ngoma za asili na sanaa za mikono
      • Kituo cha Urithi wa Ubunifu Majengo na Utalii
      • Maeneo ya kupumzika, bustani na viwanja vya michezo
      • Maeneo ya Manunuzi
      • Majengo na maeneo ya kihistoria
      • Uwanda wa bahari, fukwe na visiwa
    • Urejelezaji wa Taka Ngumu
  • Huduma Zetu
    • Vibali vya Pikipiki
    • Vibali vya Maegesho ya Teksi
    • Vibali vya Kuingiza Magari ya Mizigo
    • Vituo Vikuu vya Mabasi
    • Udhibiti Taka Ngumu
    • Taarifa za Historia ya Viwanja
    • Mazishi ya miili ya marehemu wasiokuwa na ndugu
  • Madiwani
    • Orodha ya Madiwani
    • Kamati za Kudumu
      • Kamati ya Fedha na Uongozi
      • Kamati ya Mipangomiji, Mazingira na Miundombinu
      • Kamati ya Mipango na Ufuatiliaji
      • Kamati ya Huduma za Jamii
      • Kamati ya Maadili
    • Ratiba ya Vikao vya Kisheria
    • Ratiba ya Mstahiki Meya
    • Mameya Wazamani wa Jiji
  • Miradi
    • Miradi iliyokamilika
    • Miradi iliyo kwenye Mpango
    • Miradi Inayoendelea
    • Vitega Uchumi vya Jiji
  • Machapisho
    • Sheria
    • Sheria Ndogo
    • Sera
    • Miongozo
    • Taarifa mbalimbali
    • Fomu za Maombi
    • Fomu za Ahadi ya Uadilifu
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Vyombo vya Habari
    • Maktaba ya Picha
    • Maktaba ya Video
    • Hotuba
    • Habari Mpya
    • Matukio

MSTAHIKI MEYA WA HALMASHAURI YA JIJI LA DAR ES SALAAM AKABITHI VIFAA KWA AJILI YA UJENZI WA VYOO SHULE YA MSINGI MAGOZA

Tarehe iliyowekwa: March 3rd, 2021


Na Judith Damas,                                                                                                                                                                                                                                                                                                 Mstahiki Meya wa Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam Mhe Omary Kumbilamoto ameahidi kuboresha miundombinu katika kata zote za Halmashauri ya Jiji , amesema hayo katika ziara  yake ya kutembelea shule ya msingi Magoza iliyopo  Kata ya Kisukuru   leo  tarehe 3, Machi 2021 ambapo amekabidhi vifaa vya ujenzi vyenye thamani ya shilingi laki nane na themanini (880000)  ikiwemo masinki 30  ya vyoo pamoja na  mifuko20 ya saruji hivyo  vifaa hivyo viligawanywa kama ifuatavyo,mifuko 10  ya saruji  na masinki 14 ya vyoo katika shule ya msingi Magoza pamoja na mifuko 10 ya saruji na masinki 16 ya vyoo  katika shule ya msingi Vingunguti.

Akizungumza na wananchi wa Kata ya Kisukuru  pamoja na walimu wa shule ya msingi Magoza Mstahiki Meya amemshukuru Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Dkt John Pombe Magufuli kwa kuipandisha hadhi iliyokua  Manispaa ya Ilala kuwa Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam na  kumuahidi Rais kuwa hatomuangusha.

"Namshukuru Mhe.Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt John Pombe Magufuli kwa  heshima aliyotupa na kutukabidhi Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam kutoka Manispaa ya Ilala na  sisi  kama  wasaidizi wake ni kuhakikisha tunatekeleza malengo yote ya Rais aliyokuwa nayo hivyo changamoto nyingine ndogodogo tunaahidi tutazitatua".Amesema, Meya wa Halmashauri ya Jiji la Dar es salaam.

Aidha,   Kaimu Afisa Elimu Msingi Bw.Abilah Magochi Mchia  amemshukuru Msathiki Meya wa Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam kwa kutoa msaada wa masinki 14  ya vyoo na mifuko ya simenti  10  katika shule ya msingi Magoza pamoja na masinki 16 katika  shule ya msingi Vingunguti kwani  ni msaada mkubwa ambao utaboresha maendeleo katika shule hizo .

“Tunakushukuru sana Msahiki Meya wa Halmashauri ya Jiji la Dar es salaam Mhe. Omary Kumbilamoto kwa kuleta msaada katika shule zetu za msingi za Magoza pamoja na Vingunguti ni msaada mkubwa sana ambao utaboresha shule zetu hizi kwani vyoo vya wanafunzi vilikua haviko katika kiwango kizuri lakini kwa masinki haya watoto wetu wataenda kutumia vyoo vya kisasa ambavyo vipo katika mazingira salama kwamaana hawatoweza kupata magonjwa ya maambukizi”.Amema kaimu Afisa Elimu Msingi Bw.Mchia

Sambanba na hilo, Kaimu Afisa Elimu Msingi Bw.Mchia amemshukuru  Mheshimiwa diwani Lucy Jeremiah Lugome   wa Kata ya Kisukuru  kwa kueleza Changamoto hiyo kwa Mstahiki Meya ili zifanyiwe  kazi.

“Umemueleza Mstahiki Meya Changamoto iliyokua inaikabili shule ya Msingi Magoza basi Mstahiki Meya kwa umuhimu amesisitiza kujengwa  vyumba vinne vya madarasa katika shule hii ya Msingi Magoza  na Mstahiki Meya nakuahidi hizo fedha zitaletwa hapa kwaajili ya kuanza ujenzi wa vyumba hivyo vinne vya madarasa”.Amesema  hayo Kaimu Afisa Elimu Msingi

Kwa upande wake Mwalimu Mkuu wa shule ya msingi Magoza Bw. Simeon Kahwa amesema msaada huu uliotolewa na Mstahiki Meya  utasaidia sana kuleta mazingira rafiki kwa wanafunzi kwani wataongeza idadi ya vyoo ambavyo vitasaidia kulinda afya za wanafuzi.

“Tunamshukuru sana Mstahiki Meya wa Jiji la Dar es Salaam kutuletea msaada huu kwani kimsingi idadi ya vyoo ilikua haitoshelezi kwa wanafunzi hivyo kutokana na msaada huu tutaongeza idadi ya vyoo kwa ajili ya kuleta mazingira rafiki kwa watoto wetu”.Amesema Mwl.Kahwa

Matangazo

  • TAARIFA KWA UMMA February 19, 2025
  • TAARIFA KWA UMMA - MATUMIZI YA NISHATI SAFI YA KUPIKIA January 17, 2025
  • MATOKEO YA UPIMAJI WA KITAIFA WA DARASA LA NNE (SFNA) 2024 January 04, 2025
  • UCHAGUZI WA WANAFUNZI WA KIDATO CHA KWANZA, 2025 December 16, 2024
  • Angalia zote

Habari Mpya

  • "Tutahakikisha tunasimamia Kata 36 na Mitaa 159 ili Jiji la DSM liwe safi" - DC Mpogolo

    May 03, 2025
  • Jiji La DSM laweka mikakati kushinda UMITASHUMTA ngazi ya Mkoa

    April 29, 2025
  • Wakazi wa Jiji la Dar es Salaam waadhimisha Muungano kwa kupanda miti na kufanya usafi wa mazingira

    April 26, 2025
  • Zoezi la usafi wa mwisho wa wiki laendelea

    April 12, 2025
  • Angalia zote

Video

Msimbazi Basin Development Project Implementation Area
Video Zingine

Viunganishi vya Haraka

  • Mameya wa zamani wa Jiji
  • Vibali vya kuingia na Pikipiki katikati ya Jiji
  • Udhibiti wa Taka ngumu Jijini
  • Eneo Maalum la Usafi Jijini
  • Kituo cha Urithi wa Ubunifu Majengo na Utalii
  • Uwanda wa Bahari, Fukwe na Visiwa
  • Sehemu za Kitamaduni, Ngoma za Asili na Sanaa za Mikono
  • Majengo na Maeneo ya Kihistoria
  • Maeneo ya Kupumzika, Bustani na Viwanja vya Michezo

Viunganishi Linganifu

  • BUNGE
  • Blogu ya Jiji
  • UTUMISHI
  • IKULU
  • TAMISEMI
  • IDARA YA HABARI MAELEZO

Wasomaji mbalimbali duniani

world map hits counter

Idadi ya Wasomaji

free HitCounter

Ramani ya Eneo

Wasiliana Nasi

    1 BARABARA YA MOROGORO 11882 DAR ES SALAAM

    Anuani ya Posta: S.L.P 20950

    Simu ya mezani: 0738 378 386

    Namba ya Mkononi: 0738 378 386

    Barua Pepe: info@dcc.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya Tovuti

Hatimiliki © 2017 Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam. Haki Zote Zimehifadhiwa.