• Wasiliana Nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua Pepe za Watumishi |
    • Malalamiko |
Dar es Salaam City Council
Dar es Salaam City Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Mamlaka za Serikali za Mitaa Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia ya Jiji
    • Dira na Dhamira
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati ya Halmashauri
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Idara
      • Fedha, Utawala na Utumishi
      • Ujenzi na Zimamoto
      • Udhibiti Taka
      • Mipangomiji, Mazingira na Usafirishaji
      • Afya na Huduma za Tiba
    • Vitengo
      • Mipango, Ufuatiliaji na Takwimu
      • Sheria na Usalama
      • Itifaki, Uhusiano na Umma
      • Mkaguzi wa Ndani
      • Ugavi na Manunuzi
  • Fursa za Uwekezaji
    • Shughuli za Utalii
      • Dar es Salaam Yetu
      • Misitu na Mashamba ya wanyama wafugwao
      • Sehemu za kitamaduni, ngoma za asili na sanaa za mikono
      • Kituo cha Urithi wa Ubunifu Majengo na Utalii
      • Maeneo ya kupumzika, bustani na viwanja vya michezo
      • Maeneo ya Manunuzi
      • Majengo na maeneo ya kihistoria
      • Uwanda wa bahari, fukwe na visiwa
    • Urejelezaji wa Taka Ngumu
  • Huduma Zetu
    • Vibali vya Pikipiki
    • Vibali vya Maegesho ya Teksi
    • Vibali vya Kuingiza Magari ya Mizigo
    • Vituo Vikuu vya Mabasi
    • Udhibiti Taka Ngumu
    • Taarifa za Historia ya Viwanja
    • Mazishi ya miili ya marehemu wasiokuwa na ndugu
  • Madiwani
    • Orodha ya Madiwani
    • Kamati za Kudumu
      • Kamati ya Fedha na Uongozi
      • Kamati ya Mipangomiji, Mazingira na Miundombinu
      • Kamati ya Mipango na Ufuatiliaji
      • Kamati ya Huduma za Jamii
      • Kamati ya Maadili
    • Ratiba ya Vikao vya Kisheria
    • Ratiba ya Mstahiki Meya
    • Mameya Wazamani wa Jiji
  • Miradi
    • Miradi iliyokamilika
    • Miradi iliyo kwenye Mpango
    • Miradi Inayoendelea
    • Vitega Uchumi vya Jiji
  • Machapisho
    • Sheria
    • Sheria Ndogo
    • Sera
    • Miongozo
    • Taarifa mbalimbali
    • Fomu za Maombi
    • Fomu za Ahadi ya Uadilifu
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Vyombo vya Habari
    • Maktaba ya Picha
    • Maktaba ya Video
    • Hotuba
    • Habari Mpya
    • Matukio

Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam apokea taarifa ya mpango kazi wa Anuani za makazi katika Halmashauri zote za Mkoa huo

Tarehe iliyowekwa: February 15th, 2022

Na. Judith Msuya

Kuelekea Sensa ya  watu na Makazi ya Mwaka 2022 kwa Maendeleo endelevu ya Tanzania Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Mh. Amos Makalla leo Februari 15, 2022 amefanya kikao kazi na viongozi mbalimbali wa Halmashauri tano(5) za Mkoa wa Dar es Salaam ikiwemo Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam, Halmashauri ya Manispaa ya Temeke, Halmashauri ya Maniapaa ya Kinondoni , Halmashauri ya Manispaa ya Ubungo Pamoja na Halmashauri ya Manispaa ya Kigamboni lengo likiwa kuelimisha, kuhamasisha  na kujua mpango kazi wa kwaajili ya anuani za Makazi ambazo ni msingi mzuri wa Sensa ya Makazi ya Mwaka 2022.

Kikao kazi hicho kilichofanyika katika Ukumbi wa Arnatoglou Jijini Dar es Salaam   kilichowajumuisha   viongozi mbalimbali wakiwemo Kamisaa wa Sensa ,Mwakilishi kutoka Wizara ya Habari na Mawasiliano, Wakuu wa Wilaya zote  tano, Mameya wa Halmashauri zote tano, Wakurugenzi wa Halmashauri zote, Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Mkoa wa Dar es Salaam, wataalamu wa takwimu Pamoja na maafisa Ardhi kutoka Halmashauri zote za Mkoa wa Dar es Salaam.

Aidha Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Mhe. Amos Makalla amewaelekeza wakurugenzi wa  Halmashauri zote za Mkoa wa Dar es Salaam kuharakisha mpango kazi wa oparesheni ya zoezi la anuani za makazi ambslo ndio msingi mzuri wa kufanikisha zoezi la sensea ya Wat una Makazi ya Mwaka 2022 inayotarajiwa kuanza mwezi wa nane mwaka huu.

Sambamba na hilo RC Makalla amesema zoezi hilo lina manufaa makubwa kwakua  linakwenda kuweka Jiji katika mpangilio mzuri kwani migogoro ya ardhi itapungua suala la ulinzi na usalama litaimarika, majanga ya moto yatapungua na litawezesha biashara kidijitali hivyo ametoa wito kwa wananchi kulipokea vizuri na kutoa ushirikiano ili kukamilisha zoezi hili kwa wakati.

Hata hivyo Mhe. Makalla amempongeza Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan kwa kuleta zoezi hilokwa wakati muafaka ambao una mapinduzi makubwa ya sayansi na Teknolojia na mambo mengi yanakwenda kwa mfumo wa kidijitali.

Vilevile Mhe. Makalla amewapongeza Viongozi wote wa Mkoa wa Dar es Salaam walioshiriki katika zoezi zima la kuwapanga wafanyabiashara Pamoja na maandalizi mazuri waliyoyafanya kupendezesha  na kusafisha Mkoa wa Dar es Salaam kwani Mkoa wa Dar es Salaam umekua ni miongoni mwa Majiji safi barani Afrika ambapo Mkoa wa Dar es Salaam umeshika nafasi ya sita(6) hii inaonyesha ni jinsi gani zoezi la kupendezesha na kusafisha Dar es Salaam limeweza kufanyika vizuri na kwa utaratibu mzuri.

Kwa upande wake Kamisaa wa Sensa Mhe. Anna Makinda ameeleza kua "japo zoezi hili anuani za makazi ni gumu kutokana na asili ya Mkoa wetu wa Dar es Salaam lakini nawaomba mlifanye kwa umakini mkubwa na weledi kwa kushirikiana na wataalamu wetu Wa takwimu kusudi shilingi Bilioni 28 zilizotengwa na Mhe. Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan zitumike kwa uhakika na kazi iwe nzuri na tuimalize kwa wakati japo muda ni mchache.”

Akitoa taarifa fupi kwa Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam juu ya utekelezaji wa  mpango kazi wa ukusanyaji taarifa za Anuani za Makazi Kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam Bi. Tabu Shaibu ameeleza kua Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam imejipanga vizuri katika kuratibu zoezi la ukusanyaji wa taarifa kwani   imeweza kuwajengea uwezo Watendaji wa mitaa na Kata ili waweze kusimamia  vizuri ukusanyaji wa takwimu hizo.

“Tarehe 14, Februari 2022  Halmashauri ya Jiji ilifanya Kikao na Watendaji Kata na MItaa Pamoja na Waratibu lengo ikiwa ni kuwajengea uwezo juu kusimamia zoezi zima la Anuani za Makazi Pamoja na kuwapa maelekezojuu ya kufanya kazi zilizopo chini yao, pia Kutokana na kuwa Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam ina Kata 36 na mitaa 159 ambazo zina Idadi ya  kaya 486138 hivyo ilikufanikisha kazi hii tutahitaji wakusanya data mia tatu kumi na nane (318) na  muda wa utekelezaji kulingana na mpango kazi ni siku sitini (60) hivyo tumepanga ratiba ya kuwajengea uwezo watu wote watakaohusika katika kazi hii ambapo tarehe Februari 17 tutawajengea uwezo watendaji Kata na Mitaa na februari 23, 2022 tutawajengee uwezo wakusanya taarifa namna ya kufanya kazi hiyo na  mnamo Februari 23, 2022 zoezi la kukusanya taarifa za Anuani za Makazi litaanza rasmi na hadi kufikia April 23, 2022 zoezi hilo litakua  limekamilika.”Ameeleza Bi. Tabu Shaibu.

Matangazo

  • TAARIFA KWA UMMA February 19, 2025
  • TAARIFA KWA UMMA - MATUMIZI YA NISHATI SAFI YA KUPIKIA January 17, 2025
  • MATOKEO YA UPIMAJI WA KITAIFA WA DARASA LA NNE (SFNA) 2024 January 04, 2025
  • UCHAGUZI WA WANAFUNZI WA KIDATO CHA KWANZA, 2025 December 16, 2024
  • Angalia zote

Habari Mpya

  • "Tutahakikisha tunasimamia Kata 36 na Mitaa 159 ili Jiji la DSM liwe safi" - DC Mpogolo

    May 03, 2025
  • Jiji La DSM laweka mikakati kushinda UMITASHUMTA ngazi ya Mkoa

    April 29, 2025
  • Wakazi wa Jiji la Dar es Salaam waadhimisha Muungano kwa kupanda miti na kufanya usafi wa mazingira

    April 26, 2025
  • Zoezi la usafi wa mwisho wa wiki laendelea

    April 12, 2025
  • Angalia zote

Video

Msimbazi Basin Development Project Implementation Area
Video Zingine

Viunganishi vya Haraka

  • Mameya wa zamani wa Jiji
  • Vibali vya kuingia na Pikipiki katikati ya Jiji
  • Udhibiti wa Taka ngumu Jijini
  • Eneo Maalum la Usafi Jijini
  • Kituo cha Urithi wa Ubunifu Majengo na Utalii
  • Uwanda wa Bahari, Fukwe na Visiwa
  • Sehemu za Kitamaduni, Ngoma za Asili na Sanaa za Mikono
  • Majengo na Maeneo ya Kihistoria
  • Maeneo ya Kupumzika, Bustani na Viwanja vya Michezo

Viunganishi Linganifu

  • BUNGE
  • Blogu ya Jiji
  • UTUMISHI
  • IKULU
  • TAMISEMI
  • IDARA YA HABARI MAELEZO

Wasomaji mbalimbali duniani

world map hits counter

Idadi ya Wasomaji

free HitCounter

Ramani ya Eneo

Wasiliana Nasi

    1 BARABARA YA MOROGORO 11882 DAR ES SALAAM

    Anuani ya Posta: S.L.P 20950

    Simu ya mezani: 0738 378 386

    Namba ya Mkononi: 0738 378 386

    Barua Pepe: info@dcc.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya Tovuti

Hatimiliki © 2017 Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam. Haki Zote Zimehifadhiwa.