Wednesday 27th, September 2023
@Viwanja vya Mnazi Mmoja, jijini Dar es Salaam
Magonjwa yasiyoambukiza yakiwemo shinikizo la damu, magonjwa ya moyo, saratani na kisukari yamekuwa chanzo cha vifo na usumbufu kwa wananchi wa maeneo ya mijini ikiwemo Mkoa wa Dar es Salaam.
Mienendo isiyofaa katika maisha ikiwemo kutokufanya mazoezi, ulaji usiofaa, ulevi na uvutaji sigara imekua ni sababu kuu za kuchangia kuenea kwa magonjwa yasiyoambukiza.
Serikali inaendelea kutoa elimu ya kutosha ya namna bora ya kukabiliana na magonjwa hayo na kuendelea kuboresha na kuongeza miundombinu mbalimbali ya afya
Kupitia wiki hii ya maadhimisho wananchi watapata fursa ya kupima magonjwa mbalimbali bure na kupatiwa ushauri wa kitaalamu.
1 BARABARA YA MOROGORO 11882 DAR ES SALAAM
Anuani ya Posta: S.L.P 20950
Simu ya mezani: 2128800
Namba ya Mkononi:
Barua Pepe: info@dcc.go.tz
Hatimiliki © 2017 Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam. Haki Zote Zimehifadhiwa.